Serikali imeziagiza halmashauri zote nchini kuhakikisha hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu ziwe zimekamilisha miundombinu ya vyumba vya upasuaji katika vituo vya afya.
Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dokta Khamisi Kigwangala wakati akizindua vituo 26 vya afya Mkoani Kigoma na kusema kuwa kukamilika kwa vyumba hivyo kutanusuru vifo vya watoto na kina mama wakati wa kujifungua.
Naibu Waziri Dkt Kigwangala amesema endapo halmashauri itashindwa kutekeleza agizo hilo viongozi wake watachukuliwa hatua za kinidhamu na vituo vyao vya afya Vitashushwa hadhi na kuwa zahanati.
No comments:
Post a Comment