Sunday, August 6, 2017

6 August 2017, Usain Bolt kayakanyaga

Mwanariadha Usain Bolt kutoka nchi ya Jamaica ameshindwa kutetea taji la dunia la mbio za mita 100 na kuangukia nafasi ya tatu huku Justin Gatlin kuibuka kidedea nafasi ya kwanza katika mashindano yaliyofanyika mjini London usiku wa kuamkia leo.

Gatin anayetokea Marekani ndiye bingwa mpya wa dunia wa mbio za mita 100 kwa sasa ambapo alikimbia kwa sekunde 9.92 huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Christian Coleman naye anatokea Marekani kwa kukimbia kwa sekunde 9.94 na kujipatia medali za fedha na Bolt kujinyakulia zawadi ya medali ya dhahabu kwa kukimbia kwa sekunde 9.95.

Kwa upande mwingine, mashindano hayo kwa Bolt ndiyo yalikuwa ya mwisho japo hajafanya vizuri lakini mashabiki waliyokuwepo uwanjani hapo walionekana kumshangilia kwa nguvu zaidi wakati wa kumuaga.

No comments: