Ujumbe wa usalama wa Umoja wa Mataifa (MINUSMA )nchini Mali imefanya ugunduzi wa makaburi ya halaiki katika kanda ya kaskazini ya nchi hiyo .
MINUSMA ulifanya shughuli ya ufukuaji wa makaburi hayo katika juhudi za kufanya utafiti kufuatia ripoti za kuwa na ukiukaji wa haki za kibinadamu katika kitongoji cha Anefis .
Kumekuwa na mapigano baina ya makundi kutoka jamii ya Tuareg katika wiki za hivi karibuni jambo aambalo limepelekea kuharibiwa kwa mkataba wa amani uliotiwa saini mwaka 205 .
Ujumbe huo hadi kufikia sasa umethibitisha ripoti 34 za ukiukaji wa haki za binadamu ikiwa ni pamoja na utumiaji wa watoto katika vita
No comments:
Post a Comment