Waziri wa ulinzi wa Sudan Jenerali Ivad Muhammed bin Avf amesema kuwa njia pekee ya kutokomeza vita za wenyewe kwa wenyewe zinazozidi kuikumba Sudan ni kuwanyanganya raia wote silaha wanazozimiliki.
Kwa mujibu wa habari,waziri huyo amesema kuwa ikiwezekana hata jeshi litatumia nguvu kuhahikisha kuwa silaha hizo zinakusanywa nchini kote.
Sudan imekuwa na vita za ukabila kwa muda mrefu hasa kwa sababu wananchi wengi wanamiliki silaha kirahisi.
Waziri huyo anaamini kuwa njia hiyo itaonyesha matunda hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment