Tuesday, August 1, 2017

1 August 2017, Mikoa ya Dodoma,Mwanza na Mbeya yapongezwa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameipongeza mikoa ya Dododma, Mbeya na Mwanza kwa kutekeleza agizo la serikali la kujenga Nyumba kwaajili ya Vituo vya kuwatibu walioathirika na matumizi ya dawa za kulevya katika maeneo yao.

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa pongezi hizo baada ya kuzindua nyumba maalum ya kutibu waathirika wa dawa za kulevya kutoka mikoa ya Kanda ya nyanda za juu kusini, ambayo imejengwa na Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya kwa kushirikiana na Shirika lisilo la Kiserikali Waltereed.

Mwezi Juni mwaka huu serikali imetoa maagizo kwa mikoa yote nchini kujenga nyumba maalum kwaajili ya matibabu kwa watanzania walioathirika na dawa za kulevya

Kwa upande wake kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya Rogers Sianga na Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya Dokta Godlove Mbwanji wamesema nyumba maalum ya kutibu waathirika wa dawa za kulevya itasaidia vijana kurudi katika hali zao.

Takwimu za kimatibabu za Wizara ya Afya zinaonesha kuwa waathirika wanaotumia dawa ya Methadoni hadi mwezi Juni mwaka huu imefikia 4,075 ambao wamerudi katika hali yao ya kawaida.

No comments: