Rais wa Rwanda Paul Kagame aapishwa kuhudumia nchi hiyo kwa awamu ya tatu kama rais baada ya ushindi mkubwa katika uchaguzi.
Hafla ya kuapishwa kwa rais huyo ilifanyika katika uwanja wa kitaifa jijini Kigali ambapo marais 19 wa mataifa mengine walihudhuria .
Kagame mwenye umri wa miaka 59 alichaguliwa tena kuhhwa rais wa Rwanda baada ya kuibuka mshindi katika kinyang'anyiro cha kuwaniaa urais kwa asilimia 99 ya kura .
Licha ya kuwa na ushindi mkuu katika uchaguzi wakosoaji wengi wamekuwa wakidai kwamba uongozi wa Kagame umekuwa wa ukandamizaji na ukosefu wa uhuru .
Miongoni mwa marais waliohudhuria hafla hiyo ni raiss wa Sudan Omar Al Bashir ,anayetakikana na mahakam ya kimaataifa ya Hague ,ICC
No comments:
Post a Comment