Wafanya biashara Mkoani Mbeya wameiomba serikali kutafuta suluhisho la kudumu la majanga ya moto katika maeneo ya biashara.
Maombi hayo yanakuja ikiwa ni saa kadhaa zimepita tangu moto ambao mpaka sasa haujajulikana chanzo chake kuteketeza zaidi ya Vibanda 2,000 vya wafanyabiashara katika soko la SIDO Mjini Mbeya, na kusababisha hasara ambayo haijafahamika mpaka sasa.
Baada ya moto kuteketeza maelfu ya vibanda vya wafanyabiashara katika soko la SIDO Mjini Mbeya, vikao vimeendelea kwaajili ya tathimini ya kilichojitokeza mjini Mbeya
Hata hivyo wafanyabiashara wa soko waliokumbwa na athari za moto wanatoa maombi kwa serikali juu ya majanga haya ya moto.
Halmashauri ya Jiji la Mbeya ambao ndio wamiliki wa soko hili, chini ya Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya, imewaomba wananchi wawe watulivu katika kipindi hiki kigumu.
No comments:
Post a Comment