Thursday, August 17, 2017

17 August 2017, Jengo la Yanga kupigwa mnada

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Klabu ya Simba SC, Haji Manara amefunguka na kuwapa pole watani wake wa jadi klabu ya Yanga kufuatia taarifa iliyotoka katika moja ya gazeti kuonyesha jengo lao litapigwa mnada Jumamosi ya wiki hii.

Haji Manara ametoa pole hiyo kupitia ukurasa wake wa Instgram na kuwaombea watani wao wajadi kwa kusema hivi sasa hali yao si nzuri hivyo kama jengo hilo kitauzwa watakwenda kukaa wapi.

"Mungu wangu,Jumosi hii jengo la Yanga linapigwa mnada, Wizara ya Ardhi waoneeni huruma kidogo wenzetu wana Swaumu kali, Daah!!sasa watahamia wapi? Shubamit" alimalizia Haji Manara

Mbali na hilo klabu ya Simba na Yanga zote zipo visiwani Zanzibar zikijipanga kwa ajili ya mchezo wa ngao ya jamii unaowakutanisha watani hao katika uwanja wa Taifa siku ya Jumatano ya tarehe 23 Agosti 2017.

No comments: