Thursday, August 17, 2017

17 August 2017, Wafungwa 37 wauawa gerezani wakati wa msako nchini Venezuela

Wafungwa 37 wameripotiwa kuuawa gerezani kipindi ambacho vikosi vya serikali ya Venezuela vilivamia jela moja katika jimbo la Amazonas .

Wawakilishi wa vyama vya kutetea haki za binadamu wamekuwa wakitoa malalamishi kuwa kumekuwa na makundi hatari katika gereza hizo ambao walikuwa wana silaha hatari ikiwa ni pamoja na vilipuzi.

Serikali ya Venezuela ipo katika harakati ya kuweka mamlaka katika gereza kama hizo zenye ghasia na pia kutumia misako ya ghafla katika maeneo kama hayo.

No comments: