Friday, August 18, 2017

18 August 2017, Watoto zaidi ya 100 walifariki

Watoto zaidi ya 100 miongoni mwa watu waliofariki katika mafuriko yaliotokea nchini Sierra Leone
Watoto 105 walifariki miongoni mwa watu 312 waliofariki katika mafuriko yaliotokea mjini Freetown nchini Sierra Leone.

Idadi rasmi iliotolewa na serikali baada ya mafuriko nchini Sierra Leone imefahamisha kuwa watu 312 ndio waliofariki huku wengine wasiopungua 600 hawajulikani walipo.

Nvua kali zilizonyesha nchini humo zilisababisha mafuriko na kupelekea maafa Jumatatu.

Daktari katika kitengo kinachohusika na kuhifathi maiti katika hospitali ya Connaught mjini Freetown Mohammed Sinneh Kamara amesema kuwa watoto 105 walifariki.

No comments: