Tuesday, August 1, 2017

1 August 2017, Zaidi ya raia 100 wauawa kutokana na imani potofu nchini Tanzania

Takriban watu 115 wengi wao wakiwa ni wanawake wameuawa kutokana na  imani potofu toka mwezi Januari nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa habari,kituo cha haki za binadamu kimeripoti kuwa wanawake 79 waliuawa na raia wenye hasira baada ya kuwashutumu kuhusika na uchawi.

Watu wenye macho mekundu hutuhumiwa kuwa wachawi na kushambuliwa.

Ripoti zinaonyesha kuwa wanawake katika vijiji vingi hupatwa na macho mekundu kutokana na kuvuta moshi jikoni kwa muda mrefu.

Hata hivyo imani potofu za watu wengi huwafanya waamini kuwa macho hayo ni dalili ya uchawi.
Kuuawa kwa wanawake hao ni kinyume cha haki za binadamu na vitendo hivyo hutokea hasa Mbeya na Dar es Salaam.

Msemaji wa Polisi amesema kuwa wananchi wanahitaji kupewa elimu ya msingi kuhusu suala hilo.

Hata hivyo inasemekana kuwa wananchi hujichukulia sheria mikononi kutokana na kutokuwa na imani na utekelezaji wa sheria na haki nchini.

No comments: