Saturday, June 2, 2018

JAY MOE HIP HOP NI BIASHARA

Msanii nguli wa hip hop, Jay Moe amedai kwa sasa kuna vitu vimebadilika kutoka wa wasanii wa hip hop na kuwa biashara tofauti 

Moe anafanya vizuri na wimbo ‘Bata.amebainisha kuwa .
“Sasa hivi tunawekeza sana kwenye muziki tofauti na miaka ya zamani tunatoa wimbo tu hakuna uwekezaji wowote ambao tulikuwa tunaweka,” .

“Lakini sasa hivi au miaka ya sasa hivi muziki umekuwa biashara, kwahiyo lazima pia unavyowekeza uhakikishe uwe na target nzuri ya kuweza kujua pesa yangu itarudi vipi,”. amesema Jay Moe

JOACHIM LOW AIKANA MADRID

Mkufunzi wa Ujerumani Joachim Low ameweka wazi kuwa hakuna uwezekano wa kuichua Real Madrid.

Raia wa Ureno na Mshambuliaji wa Real Madrid  Christiano Ronaldo  (33 )anataka kuichezea Manchester United


Friday, June 1, 2018

MWANZA YA PILI KWA UCHUMI

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amesema Jiji lake ni kitovu cha pili cha uchumi ukitoka Mkoa wa Dar es salaam unaochangia mfuko wa taifa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa benki ya Ecobank  jijini hapa Mongella alisema, zaidi ya shilingi Billion 4 zimetengwa kwa ajili ya kulipa fidia kwa wakazi wa eneo la Fella Wilayani Misungwi lenye ukubwa wa hekta 1500 eneo hilo litajengwa bandari ya nchi kavu ambayo reli ya standard gauge itaishia.

Mongella aliitaka Benki hiyo kutengeneza bidhaa itayoitambulisha kanda ya ziwa na kuwataka wawekezaji wengine waje Mwanza kwa kuwa ujenzi wa viwanda unaendelea na halmashauri zote zinaendelea kutenga maeneo kwa ajili ya viwanda.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Ecobank Peter Machunde aliwataka watu wanaosambaza maneno ya kuwa benki hiyo ni yakinaijeria waache kwakuwa hiyo siyo benki ya kinaijeria na kuwa Makao Makuu yake ni Togo.Aidha alisema kuwa benki ya kiafrika (Pan Africa) na sio kama wanavosema baadhi ya watu kuwa ni ya kinaijeria”alisema Machunde.

Pia alisena kuwa Benki ya EcoBank inafanya kazi kwenye nchi 35, ina matawi 1700 na matawi yaliyopo nchini ni matawi saba pekee.

HIMID MAO ATIMUKIA MISRI

Aliyekuwa nahodha wa klabu ya soka ya Azam FC, Himid Mao ameiaga rasmi baada ya kusaini kuichezea timu ya Petrojet ya Misri

''Nimeishi kama mwana familia kwa miaka yote nilikuja nikiwa kijana mdogo kabisa wa kidato cha kwanza naondoka nikiwa nimepevuka kimwili na kiakili, mimi ni binadamu kama kuna sehemu niliwakosea naombeni mnisamehe na mimi nimesamehe kama mlinikosea'', ameandika.

Himid  amewashukuru viongozi wa timu hiyo kwa kuwa imara katika nyakati zote walipokuwa wanafanya vizuri na hata walipofanya vibaya waliwapa moyo na kuwajenga ili wafanye vizuri.

LHimid Mao amesaini mkataba wa miaka mitatu wa kuichezea timu ya wauza mafuta wa Misri Petrojet ambao wamemaliza ligi wakiwa katika nafasi ya 12 msimu huu.

Himid ameondoka akiwa ameisaidia Azam FC kumaliza katika nafasi ya pili kwenye VPL

ZIDANE KUHAMIA UINGEREZA

Chelsea  iko karibuni  kumshawishi aliyekuwa mkufunzi wa Real Madrid aliyetangaza anaachia ngazi Zinedine Zidane kuwa mkufunzi wake mpya