Aliyekuwa nahodha wa klabu ya soka ya Azam FC, Himid Mao ameiaga rasmi baada ya kusaini kuichezea timu ya Petrojet ya Misri
''Nimeishi kama mwana familia kwa miaka yote nilikuja nikiwa kijana mdogo kabisa wa kidato cha kwanza naondoka nikiwa nimepevuka kimwili na kiakili, mimi ni binadamu kama kuna sehemu niliwakosea naombeni mnisamehe na mimi nimesamehe kama mlinikosea'', ameandika.
Himid amewashukuru viongozi wa timu hiyo kwa kuwa imara katika nyakati zote walipokuwa wanafanya vizuri na hata walipofanya vibaya waliwapa moyo na kuwajenga ili wafanye vizuri.
LHimid Mao amesaini mkataba wa miaka mitatu wa kuichezea timu ya wauza mafuta wa Misri Petrojet ambao wamemaliza ligi wakiwa katika nafasi ya 12 msimu huu.
Himid ameondoka akiwa ameisaidia Azam FC kumaliza katika nafasi ya pili kwenye VPL
No comments:
Post a Comment