Tuesday, May 8, 2018

SERIKALI YABAINISHA ULIPWAJI FIDIA KWA ASKARI

Serikali imesema kuwa malipo ya fidia kwa askari wanaojeruhiwa au kufariki dunia wakiwa katika shughuli ya kulinda amani kwenye nchi mbalimbali hulipwa na Umoja wa Mataifa na nchi Washirika.

Kauli hiyo imetolewa Bungeni Jijini Dodoma na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi wakati wa kipindi cha maswali na majibu.

Wizara nyingine iliyopata nafasi ya kuulizwa maswali hii leo ni ile ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, ambapo Naibu Waziri wa wizara hiyo Elias Kwandikwa ametaja mpango wa ujenzi wa barabara katika Jimbo la Same Mashariki, lengo likiwa ni kuendeleza kilimo cha Tangawizi.
Vikao vya bunge vinaendelea Jijini Dodoma. kikiwa ni kikao cha  24 mkutano wa 11.ambapo baada ya kipindi cha maswali na majibu wabunge wameendelea kujadili bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa mwaka wa fedha wa 2018/2019.

No comments: