Thursday, May 24, 2018

MERKEL ,LI KEQIANG WATETE MAKUBALIANO YA KINYUKLIA

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na waziri mkuu wa China Li Keqiang wametetea makubaliano ya kinyuklia na Iran.

Waziri mkuu  huyo wa china  amesema kusitisha makubaliano hayo kutaleta utata katika majadiliano na Korea kaskazini.

Merkel na Li walionesha msimamo wa pamoja kuelekea Iran pamoja na biashara huru, masuala mawili ambayo yameshuhudia uingiliaji kati wa Marekani

Ingawa rais Donald Trump alichukua hatua hiyo.

Hayo yalijadiliwa katika mkutano wao katika ziara ya kansela Merkel mjini Beijing.

Li alionya kwamba kusitisha makubaliano hayo na Iran, hakutaiathiri tu Iran, lakini pia kutakuwa na athari hasi katika uwezo wa kutatua masuala mengine mazito kupitia majadiliano ya amani.

Hakuitaja Korea kaskazini kwa jina , lakini wachambuzi wameonya kwamba kujitoa kwa Trump kutoka katika makubaliano hayo na Iran kunachafua uaminifu wa Marekani kabla ya mkutano uliopangwa kufanyika katika ya kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un na Trump mwezi ujao.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel pia alieleza wasi wasi wake juu ya athari za kiuchumi kwa Ulaya kutokana na hatua hiyo ya Trump kujitoa kutoka katika makubaliano na Iran.

No comments: