Kansela wa Ujerumani Angela Merkel kuelekea China kwa lengo la kibaiashara wakati China na Umoja ya Ulaya kuwa zinapambana na Marekani kuhusiana na masuala ya kibiashara pamoja na kujitoa kwa Marekani katika makubaliano ya kinyuklia na Iran.
Merkel, ambaye anatarajiwa kuondoka mchana huu, amesema katika ujumbe wake wa kila wiki kwamba mazungumzo yake na viongozi wa China yatahusisha masuala kama utawala wa sheria, hali ya uchumi na mizozo wa kimataifa kama ile inayohusu biashara.
Licha ya wasi wasi katika mahusiano na Marekani, maafisa wa Ujerumani wamesisitiza dhamira yao kuhusu mahusiano ya Ulaya na Marekani na kupuuzia maelezo kwamba Ujerumani inatafuta washirika mbadala pamoja na kuwa pamoja na Urusi na China katika suala la makubaliano ya kinyuklia na Iran na masuala mengine.
No comments:
Post a Comment