Akizungumza wakati wa uzinduzi wa wiki ya chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi kiwilaya katika kijiji cha Nyombo Wilaya ya Njombe, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Valentino Hongoli amesema wanawake wengi katika vijiji vya halmashauri hiyo wamepoteza maisha kutokana na kuamini wamerogwa.
Akisoma taarifa ya uzinduzi huo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Monica Kwiluhya amesema wanafunzi zaidi ya 1600 wanatarajiwa kupatiwa chanjo hiyo.
Akizindua wiki ya chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi Katibu Tawala Wilayani humo Jafari Simika amewataka wananchi kupata chanjo hiyo kwani pia itaokoa fedha za matibabu zinazoweza kutumika katika miradi ya maendeleo
Uzinduzi huo ni kiashiria cha kuanza kwa zoezi endelevu la chanjo Wilayani humo lenye lengo la kufanikiwa kwa zaidi ya asilimia 90.
No comments:
Post a Comment