Mrithi wa Arsene Wenger kama meneja wa Arsenal itabidi atumei bajeti ndogo msimu huu wa joto ya kiasi ya £ milioni 50
Mkurugenzi mtendaji wa Arsenal Ivan Gazidis anaamini kuwa kapteni wa zamani wa Gunners Mikel Arteta, mwenye umri wa miaka 36, ambaye sasa ni kocha katika timu ya Manchester City, huenda akawa ndiye mrithi wa Arsene Wenger. (Sky Sports)
Aliyekuwa mchezaji wa kiungo cha kati wa Arsenal Ray Parlour anaamini kuwa Meneja wa Newcastle Rafael Benitez huenda ndiye anayestahili kumrithi Arsene Wenger.

(Talksport)
Arsene Wenger huenda atakuwa na nia ya kuisimamia timu ya taifa ya England siku moja anasema mwandishi wa soka ya Ufaransa Julien Laurens. (BBC Radio 5 live)
No comments:
Post a Comment