Friday, April 20, 2018

20 APRIL 2018,SERIKALI KUKARABATI MIUNDOMBINU YOTE ILIYOATHIRIWA NA MVUA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema serikali itahakikisha inafanya ukarabati wa miundombinu iliyoharibika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha baada ya kamati za maafa za mikoa kutathmini uharibifu uliosababishwa na mvua.
Majaliwa ametoa kauli hiyo bungeni mjini Dodoma wakati akijibu maswali ya papo kwa hapo ikiwa ni utaratibu uliowekwa na bunge unaomtaka Waziri Mkuu kutumia siku ya alhamisi kujibu maswali mbalimbali ya wabunge.
Miongoni mwa swali lilijitokeza ni uharibifu wa Miundombinu uliosababishwa na mvua ambapo Waziri Mkuu amebainisha taratibu zitakazotumika kurejesha miundombinu iliyoharibika
Waziri Mkuu pia amewataka baadhi ya wabunge kuacha siasa kuhusu hatua zinazochukuliwa na serikali za kuhamisha watu wanaoishi mabondeni.
Katika hatua nyingine Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amewasilisha bungeni bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka 2018/2019  na kusema wizara hiyo imejikita kuboresha upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na kuimarisha matibabu ya kibingwa.
Akiwasilisha maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge huduma za jamii,mwenyekiti wa kamati hiyo Peter Serukamba ameishauri wizara kuangalia upya suala la usambazaji dawa nchini.

No comments: