Wananchi kisiwani Pemba wametakiwa kuondosha hofu kwa kudhani kuwa utaratibu umiliki na uhaulishaji wa ardhi umeletwa kwa ajili ya kuwadhulumu badalayake waelewe kuwa umekuja kuondoa changamlto ya migogoro inayoibili sekta hiyo
Wametakiwa kufahamu kwamba utaratibu huo upo kisheria kwa sheria namba 12 ya mwaka 1992 na lengo kuu ni kutoa haki na dhamana kwa mwenye kumiliki rasilimali hiyo
Hayo yamekuja kufuatia wananchi wengi waliofikiwa na taluma ya kujua umuhimu wa umuliki na uhaulishaji ardhi huko Mkoani Micheweni na Makangale kuitilia mashaka sheria hiyo kwa madai kwamba utekelezwaji wake utaiondoa haki ya umiliki kwa wanyonge na kutumbukia kwa wajanja wenye vyeo na fedha
Mapema akielezea lengo la elimu hiyo Mratibu wa Bodi ya uhaulishaji Ardhi Zanzibar Dr Abdul-Nasser Hikmany amesema ni kuhamasisha jamii kufuata taratibu za umiliki jambo ambalo litasaidia kupata dhamana na kupunguza migogoro ya ya ardhi iliyodumu muda mrefu.
Naye mwanasheria wa bodi hiyo Hassan Nassor Hassan amesema jamii ni lazima ikubali kufuata sheria na mwenendo wa taratibu za Serikali katika kuwawekea mazingira mazuri ya usimamizi wa shughuli zao.
No comments:
Post a Comment