Tuesday, March 27, 2018

27 March 2018,Hati chafu iliyosababisha wakurugenzi wa Halmashauri za Kigoma, Kigoma Ujiji na Pangani kusimamishwa kazi

Rais Dkt. John Magufuli ameagiza kusimamishwa kazi kwa wakurugenzi wa Halmashauri za Kigoma, Kigoma Ujiji na  Pangani baada ya kubainika kuwa na hati chafu.
Rais Magufuli ametoa maagizo hayo Ikulu Jijini Dar es salaam, baada ya kupokea ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali (CAG\) Profesa Juma Assad huku akiagiza mawaziri kusoma ripoti hiyo ili kuhakikisha changamoto zilizoonekana katika ripoti hiyo hazijirudii.
Ripoti hiyo ambayo ukaguzi wake umewekwa katika vipengele vitatu ikiwemo hati safi, hati ya mashaka na hati chafu imezitaja Halmashauri za Kigoma, Kigoma Ujiji na Pangani kuwa na hati chafu.
Baada ya kusikiliza ripoti hiyo Rais Magufuli ametoa maagizo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tamisemi, Selemani Jaffo kuwasimamisha kazi wakurugenzi wa Halmashauri hizo.
Naye Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaahidi viongozi wa kamati za bunge kufanyia kazi mapendekezo yao.
Ripoti ya CAG imeainisha deni la taifa limefikia shilingi trilioni 46.

No comments: