Thursday, March 1, 2018

1 March 2018,Arsene Wenger, ang'ang'ania kubaki Emirate

Uongozi wa timu ya Arsenal wamemgeukia meneja wao, Arsene Wenger na kuanza kuorodhesha majina mbadala kuchukua nafasi yake.

Wenger anasema "atapindua dunia chini juu" ilikubaki kama meneja wa Arsenal
Kazi yake katika timu hiyo iliwekwa utatani wakati alipokataa kudhibitsha kama ataendelea na mkataba wake unaoisha 2019. (Mirror)

Aliyekuwa rais wa timu ya Barcelona Joan Laporta, amesema anawahimiza Arsenal kumfikiria Thierry Henry kama mbadala wa Wenger.(Telegraph)

West Ham iko tayari kumsiani mlinzi wa Ireland Kaskazini Jonny Evans, 30, kwa paundi milioni tatu kutoka kwa West Brom ikifika mwisho wa msimu. (Birmingham Mail)

Kiungo wa Arsenal na timu ya England, Jack Wilshere, 26 anasema atatoka kwenye klabu hiyo kati kati ya mwaka huu, wasipo mpatia mkataba bora zaidi. (Sun)

No comments: