Friday, February 9, 2018

9 February 2018,URUSI - Yauita uwepo wa Marekani Syria nikizuizi kikubwa cha kuleta amani

Urusi imeuita uwepo wa Marekani nchini Syria kuwa sio wa halali na kizuizi kikubwa cha kuleta amani nchini Syria.

Moscow imeishutumu Marekani kwa kuwahifadhi magaidi nchini Syria.

Msemaji wa masuala ya nje wa Urusi Maria Zaharova amesema kuwa Marekani inaharibu harakati za kuleta amani nchini Syria na ni kizuizi cha umoja na uadilifu wa taifa hilo.

Zaharova ameongeza kuwa kusema kuwa Marekani inawasaidia wahalifu na magaidi nchini Syria kutokamatwa na majeshi ya nchi hiyo na hivyo kuendeleza mashambulizi.

Uturuki nayo imelalamika kuwa Marekani inatoa silaha kwa magaidi wa PKK/PYD nchini Syria.

No comments: