Sunday, February 4, 2018

4 February 2018,Arsenal yaingia katika vita ya kuitafuta saini ya Riyad Mahrez

Arsenal inatarajiwa kujiunga katika kuwania kumsajili mchezaji wa kiungo cha kati wa Leicester Riyad Mahrez, mwenye umri wa miaka 26. (Daily Star Sunday)

Meneja wa Leicester Claude Puel anasaema "hamfikrii" Mahrez, ambaye hajaonekana katika kalbu hiyo tangu pendekezo la uhamisho wake kwenda Manchester City litibuke kufuatia kuwadia kwa muda wa mwisho wa uhamisho. (Mail on Sunday)

Muungano wa wachezaji soka kitaaluma umejitolea kusaidia kutatua hali baina ya mchezaji raia wa Algeria Mahrez na timu ya Leicester City. (Sun on Sunday)

Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich anafikiria kumlipia Maurizio Sarri Euro milioni 8 katika mkataba wake ili aweze kumsajili kocha huyo wa Napoli kuwa meneja mpya wa timu yake.(La Gazzetta dello Sport - in Italian)

Huenda bosi wa Chelsea Antonio Conte akafutwa kazi iwapo upande wake utashindwa na Watford Jumatatu. (Sunday Express)

Conte ameiambia Chelsea kuwa wanaihitaji kuwasajili wachezaji wawili au watatu wa kiwango cha kimataifa kuweze kulinyanyua taji la ligi msimu ujao, na ametaja kuwasili kwa wachezaji wengi kama mojawapo ya kushindwa kwao kulilinda taji lao msimu huu. (Sunday Telegraph)

Kipa wa Manchester City mwenye umri wa miaka 30, Joe Hart, aliyechukuliwa kwa mkopo huko West Ham, atalengwa na Chelsea iwapo Thibaut Courtois, mwenye umri wa miaka 25 ataondoka katika klabu hiyo msimu huu wa joto. (Sun on Sunday)

No comments: