Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa Marekani imekuwa ikitoa msaada kijinga Pakistan.
Kwa mujibu wa habari,rais Trump anadai kuwa Marekani imetoa msaada wa zaidi ya $33 billioni Pakistan,ndani ya miaka 15 bila ya kupata kitu chochote.
Rais Trump amesema ni wakati wa kusitisha msaada huo.
Katika mtandao wake wa twitter,rais Trump ameandika kuwa Marekani itaacha kutoa msaada Pakistan kwani ni nchi ambayo imekuwa ikitoa hifadhi kwa magaidi wanaotafutwa Afghanistan.
Trump amedai Pakistan inadhani viongozi wa Marekani ni wapumbavu na imekuwa ikiwadanganya kila kukicha.
No comments:
Post a Comment