Manchester City wameamua kuacha kutafuta mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez.
Taarifa zinasema klabu hiyo imeamua kufanya hivyo baada ya kuwa itakuwa ghali sana kuendelea kutaka kumnunua mchezaji huyo raia wa Chile mwenye miaka 29.
Meneja Pep Guardiola, mmiliki wa klabu hiyo Khaldoon al Mubarak na maafisa wengine wakuu wa klabu hiyo wote wamekubaliana na msimamo huo.
Inaarifiwa kwamba ujira anaotaka Sanchez utamfanya kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi miongoni mwa wachezaji wa City iwapo atahamia klabu hiyo.
Hili ni jambo ambalo klabu hiyo haiko tayari kufanya.
No comments:
Post a Comment