Monday, January 1, 2018

1 January 2018,Kim Jong Un-Korea kaskazini ipo tayari kutumia silaha zake za nyuklia

Kim Jong Un katika runinga ya taifa ya Korea-Kaskazini amesema kuwa taifa lake lipo tayari kutumia bomu lake la nyuklia na kusema kuwa makombora yake ya masafa marefu yanayouwezo wa kufika katika ardhi ya Marekani Popote pale.

Kim Jong Un amesema kuwa Marekani haina uwezo wa kutushambulia kwa kuwa sasa Korea-Kaskazini inaouwezo wa makombora ya nyuklia ya masafa marefu na ufunguo wake tayari upo mezani.

Kim Jong Un ameendelea kusema kuwa mazungumzo na Korea-Kusini yanawezekana na mlango upo wazi.

Kwa kumalizia Kim Jong Un amesema kuwa anataraji kutuma tume Korea-Kusini kujadili kuhusu Korea-Kaskazini kushiriki katika michezo ya olimpiki ya msimu wa baridi inayotarajiwa ifikapo Februari.

No comments: