Mbele ya Mhe Jaji Edson Mkasimongwa sheikh Ponda Issa Ponda ameibwaga Jamhuri katika rufaa dhidi yake iliyokatwa na Mkurugenzi wa mashitaka akipinga hukumu iliyomwachia huru huko mkoani Morogoro mwaka 2015 katika mashitaka matatu ikiwemo kuchochea watu kutenda kosa la mkusanyiko usio halali na kukiuka amri ya mahakama.
Mhe Jaji alikubaliana na hoja za mawakili wa sheikh Ponda Juma Nassoro, Abubakar Salim na Hamidu Ubaid kuwa upande wa mashitaka haukuthibitisha mashitaka yao wakati wa usikilizwaji wa kesi kule Morogoro na pia hata hati ya mashitaka ilikuwa na mapungufu hasa shitaka la kwanza.
Mhe Jaji alisema haikuwa sahihi kumshitaki Sheikh Ponda kwa madai ya kukiuka amri ya mahakama ya kisutu katika mahakama ya Morogoro badala yake Sheikh ilitakiwa apelekwe pale Mahakama ya Kisutu ajieleze tu lakini kwasababu ambazo hazijawekwa wazi DPP aliamua kufungua kesi mpya kitu ambacho hakipo kwenye sheria.
Mhe Jaji alisema maneno yanayodaiwa kuwa ya uchochezi hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kuchochewa nayo lakini pia ukiyasoma hayo maelezo hayatengenezi kosa lolote la jinai.
No comments:
Post a Comment