Thursday, December 14, 2017

14 December 2017,Ifahamu hatima ya mji wa Jerusalem iliyotolewa leo na Bunge la Uturuki

Bunge la Uturuki latolea wito ulimwengu mzima kutambua mji wa Jerusalem-Mashariki kama mji mkuu wa Palestina

Nyaraka uliokuwa na wito iliandaliwa na chama tawala cha AK kwa ushirikiano na chama cha upinzani cha CH na MHP ikitoa wito kwa ulimwengu mzima kuutambua mji wa Jerusalem -Mashariki kama mji mkuu wa Palestina.

Wito huo ulisomwa na Ayşenur Bahçekapılı.

Wito huo kwa ulimwengu kutambua mji wa Jerusalem-Mashariki kama mji mkuu wa Palestina umetolewa na kufahamisha kuwa mipaka iliowekwa mwaka 1967 na azimia la Umoja wa Mataifa ndio sahihi.

Mji wa Jerusalem-Mashariki umekaliwa kimabavu na Israel na kukiuka maazimia ya kimataifa  kwa miaka 50.

No comments: