Jeshi la Polisi Dar es salaam litakua likifanya doria kwa njia yaHelikopta kupiga macho na kujuahali halisi ya mitaani kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha.
Kwa mujibu wa chombo kimoja cha habari hapa chini ,Naibu Kamishina wa Polisi kikosi cha anga anaelezea.”Jukumu kubwa la Jeshi la Polisi ni kulinda usalama wa raia na mali zao na kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha Jijini Dar es salaam, na kuhatarisha maisha ya raia na mali zao, hatutaki kusikia hizi taarifa kupitia vyombo vingine, ndio maana tumeamua kutumia Helikopter ili kuona eneo kubwa zaidi.
Helikopta hii inatusaidia kuona kwa ukubwa zaidi tukiwa juu n tunapokuwa tunaona tatizo tunawasiliana na wenzetu walio chini hili kutoa msaada sehemu Husika”
No comments:
Post a Comment