Watu wasiopungua 26 wamethibitika kuuawa baada ya mtu mmoja kuvamia kanisani na kuanza kushambulia waumini kwa risasi wakati ibada ikiendelea jana huko Southerland, Texas, Marekani.
Mtuhumiwa wa shambulio hilo ametambuliwa kuwa ni Devin Patrick mwenye umri wa miaka 26.
Hata hivyo, Rais wa Marekani Donald Trump akiwa ziarani Tokyo, Japan amelaani tukio hilo na kusema mtuhumiwa huyo ni ‘mwendawazimu.’
Mamlaka huko Texas zinaelezea kuwa watu 20 waliojeruhiwa katika tukio hilo wana umri wa kati ya miaka mitano hadi 72.
Kwa mujibu wa CNN, miongoni mwa waliouawa ni msichana wa miaka 14 niu mtoto wa Mchungaji wa Kanisa la First Baptist, Frank Pomeroy.
Kituo hicho cha television kupitia mtandao wa Twitter kimesema kuwa watu wote waliofariki kwenye shambulio hilo ndugu.
Admit Habarileo
No comments:
Post a Comment