Takriban watu nane wameripotiwa kupoteza maisha huku wengine saba wakiwa wamejeruhiwa vibaya katika maporomoko ya ardhi kaskazini mwa Pakistan.
Kwa mujibu wa habari,tukio hilo limetokea wakati kundi la watoto likikusanya udongo maeneo ya Bajaur.
Ripoti zinaonyesha kuwa wengi wao waliopoteza maijsha ni watoto huku mmoja akiwa ni mwanamke.
Majeruhi wamefikishwa hospitali kwa ajili ya matibabu.
Operesheni ya uokoaji imeanza rasmi.
No comments:
Post a Comment