Friday, November 3, 2017

3 November 2017, Job Ndugai aiandikia barua NEC kuhusu jimbo la Nyalandu

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai leo Novemba 3, 2017 amemuandikia barua Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini (NEC) kumtaarifu kuwa jimbo la Singida Kaskazini lipo wazi kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo.

Taarifa ya Bunge iliyotolewa leo inasema kuwa jimbo hilo lipo wazi kutokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumfuta Uanachama Lazaro Nyalandu toka Oktoba 30, 2017 mwaka huu.

Mbunge huyo alitangaza mwenyewe kupitia vyombo vya habari kujivua nafasi zake ndani ya chama hicho na kusema kuwa ameandika barua kwa Spika kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge kupitia CCM.

No comments: