Waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras ametangaza siku ya maomboleza baada ya maafa yaliotokea kufuatia mafuriko mjini Athens.
Taarifa zilizotolewa na waziri wa afya ni kwamba watu 15 walifariki katika mafuriko yaliotokea Magharibi mwa jji la Athens baada ya mvua kubwa kunyesha.
Miongoni mwa watu waliofariki katika mafuriko hayo wamo wanawake watano.
Mkutano wa dharusha umetolewa wito na waziri mkuu wa Ugiriki ili kuendesha shughuli za uokoaji .
Katika hotuba yake katika kituo cha runinga cha taifa, waziri mkuu ametangaza siku ya maombolezo.
No comments:
Post a Comment