Yanga inadaiwa kuwa katika kigumu cha kuyumba kwa uchumi jambo ambalo sasa limetafsiriwa kukwama hata kuwamalizia baadhi ya wachezaji wao fedha za usajili akiwemo kipa Beno Kakolanya waliyemsajili kutokea Prisons.
Madai hayo yameelezwa kwamba yamechangia kwa kiasi fulani kipa huyo kushindwa kufanya vyema ingawa maelezo mengine ni kwamba alikuwa anaumwa na hata mechi yao na Singida United bado alikuwa akisumbuliwa na malaria.
Meneja wa mchezaji huyo, Selemani Haroub alisema atawasilisha barua rasmi katika klabu ya Yanga ili kudai madai hayo ya fedha yaliyobaki ambayo imeelezwa kwamba kwa utaratibu wa kawaida Yanga wamevunja mkataba wa Beno kwani wameenda kinyume na makubaliano yao.
"Ni kweli tunawadai Yanga fedha ya usajili iliyobaki, mara kadhaa tumekuwa tukiwakumbusha kwa njia ya mdomo tukiamini kwamba watashughulikia ila imekuwa ngumu hivyo tunawaandikia barua rasmi na kuwapa muda wawe wamelifanyia kazi.
Admit Mwanaspot
No comments:
Post a Comment