Kikosi cha wanajeshi wa mizinga na makombora wa Yemen huku wakishirikiana na makundi ya kujitolea ya wananchi wamejibu mashambulizi ya Saudi Arabia kwa kushambulia maeneo waliko mamluki wa Saudia huko Najran, Jizan na Asir kusini mwa Saudi Arabia.
Wanajeshi wa Yemen wamevishambulia kwa makombora ya katyusha vituo vya mamluki wa Saudia huko al Sadis na al Shorfah katika mji wa Najran.
Kikosi cha makombora cha wanajeshi wa Yemen kimevishambulia pia vituo vinne vya kijeshi katika maeneo mawili ya Jizan na Asir.
Idadi ya mamluki wa Saudia waliouliwa katika mashambulizi hayo bado haijafahamika hadi sasa.
Wakati huo huo mashambulizi ya karibuni yaliyofanywa na ndege za kivita za Saudia huko Yemen katika maeneo ya raia katika mkoa wa Saada kaskazini mwa Yemen yamejeruhi raia kadhaa akiwemo mtoto mmoja.
Ndege hizo za kivita za utawala wa Aal Saud zimeushambulia pia mji wa Nahm katika mji mkuu wa Yemen Sana'a.
No comments:
Post a Comment