Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kamishina Msaidizi wa Polisi Fortunatus Musilim amewataka abiria kutoa taarifa za madereva wanaokiuka sheria za usalama barabarani zikiwemo kuchanganya abiria na mizigo.
Kamanda Musilim ametoa kauli hiyo Jijini Dar es salaam wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari kuhusu ajali iliyotokea jana Wilayani Nkasi Mkoani Rukwa na kusababisha vifo vya watu kumi na wanne na majeruhi tisa.
Aidha Kamanda Musilim amewataka madereva kufuata sheria za usalama barabarani bila kujali muda kwani ajali za barabarani zimekuwa zikipoteza maisha ya watu wengi.
No comments:
Post a Comment