Wednesday, October 4, 2017

4 October 2017, RAIS MAGUFULI:Kubana matumizi imesaidia kutekeleza miradi ya maendeleo

Rais Dkt John Magufuli amesema kufuatia serikali kubana matumizi yasiyo na tija imeweza kufikia malengo ikiwemo utekelezaji wa mradi mpya wa umeme ili kuhakikisha azma ya uchumi wa viwanda inafikiwa.

Akizungumza jijini Dar es salaam katika mkutano mkuu wa 33 Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), Rais Magufuli amebainisha kuwa azma ya viwanda haiwezi kufikiwa endapo hakuna umeme wa kutosha.

Akizungumza wakati akimkaribisha mgeni rasmi Rais Dkt. John Magufuli, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema watendaji wa serikali za mitaa ni wasimamizi wakubwa wa miradi ya maendeleo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa ALAT- Taifa, DIWANI Gulamfaheef Abubakar Mukadam amebainisha umuhimu wa sekta ya viwanda katika mapato ya Taifa

Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) unaofanyika kwa siku mbili ukibeba kauli mbiu ya "Ardhi kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa ni Chachu ya Maendeleo, Halmashauri Zitenge Ardhi kwa ajili ya Uwekezaji wa Viwanda Vidogo na Vikubwa"

No comments: