Monday, October 2, 2017

2 October 2017,Majaliwa awataka viongozi wa Dini nchini kuthabiti amani na utulivu

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaomba viongozi wa Jumuiya na Taasisi zote za kidini nchini kuhakikisha wanawapiga vita watu wanaopanga kuvuruga amani na utulivu uliopo nchini kwa kuwa wanakwamisha maenndeleo.

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa kauli hiyo wakati akifungua mkutano Mkuu wa mwaka wa 48 wa Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya uliofanyika katika eneo la Kitonga wilayani Ilala Jijini Dar es salaam.

Amesema kuwa serikali inaelewa kuwa dini ni miongoni mwa vyanzo muhimu vya maendeleo kwa kuwa inatoa elimu ya maadili mema yenye kuwafanya waumini waepukane na maovu mbalimbali.

No comments: