Idara ya uhamiaji mkoani Kigoma imewakamata na kuwarudisha kwao raia Mia Mbili Kumi na Watatu kutoka katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo walioingia nchini kinyume cha sheria kwa madai ya kujifanya wakimbizi.
Afisa uhamiaji mkoa wa Kigoma, - Iremigius Pesambili amesema baada ya uhamiaji kuwahoji raia hao ambao wengi wao ni watoto wamejiridhisha kuwa hawana sifa za kupewa hifadhi kama wakimbizi.
Aidha idara ya uhamiaji imetoa angalizo kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri katika ziwa Tanganyika kuacha mara moja tabia ya kuwasafirisha wahamiaji kinyume cha sheria.
Kwa mujibu wa Naibu kamishna wa uhamiaji mkoa wa Kigoma Remigius Pesambili, vitendo vya ya raia kutoka katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kuingia nchini wakijifanya wakimbizi vimeongezeka hasa katika kipindi hiki ambacho zoezi la kuwarejesha kwa hiari wakimbizi kutoka nchini Burundi linaendelea.
No comments:
Post a Comment