Friday, October 13, 2017

13 October 2017,Watu wawili wanaosadikika kuwa majambazi wauawa Mbezi Jijini Dar es salaam

Watu Wawili wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wameuawa katika majibizano ya risasi na askari polisi katika eneo la MBEZI –Mshikamano Jijini Dar es salaam.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa amewaambia Waandishi wa habari kuwa moja ya watu hao waliouawa anadaiwa kumjeruhi kwa risasi Meja Jenerali Mstaafu Vincent Mritaba mwezi Septemba mwaka huu.

Kuhusu watu ambao wamekua wakifanya vitendo vya uhalifu Jijini Dar es salaam, Kamanda Mambosasa ameonya kuwa watachukuliwa hatua kali endapo wataendeleza vitendo hivyo.

No comments: