Monday, September 4, 2017

4 September 2017, Mteka watoto Arusha,Geita ashikiliwa na Jeshi la Polisi_Mponjoli

Polisi Mkoani Geita wanamshikilia kijana Samson Petro (18) mkazi wa Katoro wilayani Geita mkoani hapa Kwa tuhuma za kuteka watoto katika mikoa ya Arusha na Geita

Kijana huyo amekamatwa usiku wa Septemba 2 ,saa mbili usiku katika nyumba ya kulala wageni ya Shitungulu iliyopo mji mdogo wa Katoro.

Kamanda wa polisi mkoani hapa , Mponjoli Mwabulambo amethibitisha kukamatwa Kwa kijana huyo na kusema polisi linaendelea na uchunguzi na utakapokamilika atafikishwa mahakamani.

No comments: