Sunday, September 3, 2017

3 September 2017, Msangi:Makampuni ya ulinzi yanatakiwa kuajiri watu waliopata mafunzo

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amewataka wamiliki wa kampuni za ulinzi kuajiri watu wenye sifa na waliopata mafunzo ya ulinzi.

Akizungumza Jijini Mwanza, Kamanda Msangi amesema kumekuwepo na walinzi ambao wanashirikiana na majambazi kufanya uhalifu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tsia Taifa, Felex Kagisa amesema wamejipanga kuboresha mfumo wa uandikishaji wa walinzi ili kupata walinzi wenye weledi.

No comments: