Sunday, September 3, 2017

3 September 2017, Kenyatta: Mahakama haikutumia busara

Uhuru Kenyatta aliyekasirishwa kupita kiasi na uamuzi wa majaji wa mahakama ya juu kufuta matokea ya urais amesema kuwa mahakama hiyo ina matatizo na inahitaji kushughulikiwa.

Rais Kenyatta japokuwa ameahidi kuuheshimu uamuzi uliotolewa na mahakama hiyo,amesema ni lazima ataichukulia hatua mahakama hiyo baada ya kuchaguliwa mara ya pili.

Mahakama ya juu ilifuta matokeo ya urais siku ya Ijumaa na kusema kuwa yalikuwa na hitilafu.

Kwa mujibu wa habari,Kenyatta katika hotuba yake aliyotoa baada ya matokeo hayo kufutwa amesema kuwa haelewi ni vipi matokeo ya maseneta,magavana na kadhalika yamepitishwa isipokuwa dosari imeonekana kwenye matokeo ya urais tu.

Rais Kenyatta amesema kuwa uamuzi uliotolewa na majaji hauna mantiki hata kidogo.

Uchaguzi mkuu unatarajia kufanyika kwa mara nyingine ndani ya siku sitini zijazo.

No comments: