Thursday, September 21, 2017

21 September 2017,Watu takriban 12 wamekufa ,100 hawajulikani walipo baada ya mafuriko kutokea Kongo

Watu takriban 12 wamepoteza maisha huku wengine 100 wakiwa hawajulikani walipo baada ya mafuriko kutokea kaskazini mwa Kivu nchini Kongo.

Kwa mujibu wa habari,mafuriko hayo yamesababishwa na mvua kubwa ilionyesha usiku wa kuamkia Jumatano.

Ripoti zilizotolewa na polisi ni kwamba nyumba mia moja zimeangamizwa na mafuriko hayo baada ya mito ya Mumba na Osso kufurika.

Watu wengine 16 wanaendelea kupata matibabu baada ya kujeruhiwa katika mafuriko hayo.

Mafuriko yamekuwa yakitokea mara kwa mara kila mwaka na kusababisha vifo vya wengi mashariki mwa Kongo.

No comments: