Wednesday, September 20, 2017

20 September 2017,WAZIRI MKUU:Viongozi wa ngazi zote nchini washirikiane na serikali kuimarisha ulinzi

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza viongozi wa ngazi zote zote nchini kushirikiana na serikali kuimarisha ulinzi katika maeneo yao ili kuwafichua watu wanaoendesha vitendo vya uhalifu.

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa agizo hilo mkoani Pwani wakati wa ziara ya siku moja aliyoifanya katika mkoa huo kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda cha kutengenezea sabuni ya unga cha Keds kilichopo katika eneo la Tamko mjini Kibaha na kiwanda cha marumaru cha Tryford cha wilayani Chalinze.

Akizungumzia suala la ujenzi wa viwanda Waziri Mkuu Kasim Majaliwa amesema serikali itaendelea kuboresha na kuweka mazingira mazuri ambayo yatawavutia wawekezaji wengi kuja kuwekeza hasa kwenye sekta ya viwanda.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo amemuomba Waziri Mkuu awasaidie katika upatikanaji wa nishati ya umeme ya kutosha ili kuweza kuendesha viwanda katika mkoa huo.

No comments: