Chama tawala nchini Burundi kimelalamikia
ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyoitaka Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu
(ICC) ifanye uchunguzi kuhusu jinai zilizofanywa na viongozi wa Burundi
dhidi ya raia wa nchi hiyo.
Chama tawala Burundi kilieleza kuwa ripoti ya Umoja wa Mataifa inayosema kuwa viongozi wa
Burundi wamehusika katika kukiuka haki za raia wake kuwa ni ripoti ya
kisiasa na yenye lengo la kutoa pigo kwa chama hicho tawala.
Kuhusiana na suala hilo Evariste
Ndayishimiye Katibu Mkuu wa chama tawala cha Burundi amezishambulia kwa
maneno Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya kufuatia ripoti hiyo yenye
kukinzana dhidi ya viongozi wa Burundi na kuitaja Ulaya na nchi za
magharibi kuwa ni mashetani wa Ulaya.

No comments:
Post a Comment