Mwanza. Baada ya kucheza mechi zake tatu kwenye viwanja vya ugenini, uongzo wa ya Mbao FC, sasa umesema kuwa unarudi uwanja wake wa nyumbani CCM Kirumba kuhakikisha Simba haitoki salama.
Mbao imeanzia ugenini katika mechi zake tatu na kubahatika kupata pointi tatu na mechi ijayo inatarajia kuwa uwanja wake wa nyumbani kuwakaribisha Simba Septemba 21 mwaka huu.
Timu hiyo katika michezo mitatu ilizowahi kukipiga na Wekundu hao, haikuwahi kupata matokeo mazuri na badala yake imekuwa ikichezea vichapo.
Meneja wa Mbao FC, Faraji Muya alisema kuwa kwa sasa nguvu zao wanazielekeza kwenye mchezo wao dhidi ya Simba na kusema kuwa watahakikisha wanashinda ili kuvunja rekodi.
No comments:
Post a Comment