Shirika la Afya duniani WHO na mamlaka ya DRC wametoa taarifa kuwa majimbo 20 kati ya 26 nchini humo yamethiriwa na gonjwa la kipindupindu.
Ripoti zinaonyesha kuwa ni zaidi ya watu 500 wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa huo.
Kwa mujibu wa habari,shirika la WHO limetoa ripoti kuwa hali inazidi kuwa mbaya nchini humo toka mwishoni mwa mwezi Julai.
Wizara ya afya ya DRC imejielezea kuwa tayari imeandaa mbinu mbadala za kuudhibiti ugonjwa huo.
WHO imetangaza kuwa imetoa mchango wa zaidi ya dola za kimarekani 400,000 katika kusaidia maeneo yaliyoathirika,
No comments:
Post a Comment