Tuesday, August 8, 2017

8 August 2017, Serikali yangu haimwagi fedha _Rais Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuna baadhi ya watu wenye wivu wanaponda jitihada zake za kukwamua nchi kiuchumi , huku wakilaumu serikali kuwa hakuna pesa na kuwaonya kuwa serikali yake haitagawa fedha.

Rais Magufuli ameyasema hayo alipokuwa akihutubia Taifa mkoani Tanga ambako alikuwa kwenye ziara yake ya siku 5, na kusema kuwa watu wengi ambao wanalalamika walizoea kudhulumu wananchi na kutapeli, lakini kwa sasa haruhusu kitendo hicho kiendelee kutokea, na atakayehitaji fedha lazima aifanyie kazi.

“Wapo watu wamejaa wivu mioyoni mwao, wengine atasimama mbona hela hazipo, wale walizoea hela za rushwa, walizoea hela za utapeli, kwa sasa wanafikiri fedha hizo zitapatikana kama zamani, kwa sasa hela za utapeli za kudhulumu wananchi hazitapatikana , na nataka niwaambie na nitangaze kwa dhati kabisa, serikali yangu haigawi hela”, alisema Rais Magufuli.

Rais Magufuli aliendelea kwa kuwasisitiza wananchi kufanya kazi kihalali, na wale wataoendelea kufanya ufisadi watakiona cha mtemakuni.

“Usipofanya kazi hata hizo ulizonazo zitapotea, kwa hiyo mafisadi wakae wakijua hilo, zile fedha walizokuwa wamezoea kuzipata kwa kufisadi wananchi masikini hawatazipata tena, na wakifanya ufisadi kwa sasa hivi wajiandae kutumbuliwa na kwenda gerezani, wakaone shida ya kule, kwa sababu hatuwezi tukaruhusu Watanzania kuishi maisha ya shida, wakati wapo watu wengine walikuwa wanaishi kwa jasho la masikini”, alisema Rais Magufuli.

No comments: